Back to Home Page of CD3WD Project or Back to list of CD3WD Publications

CLOSE THIS BOOKA Guide to Make your Own Maendeleo One-pot Jiko - Jinsi ya Kujitengenezea Jiko la Maendeleo la Kutosha Chungu Kimoja (GTZ, 16 p.)
VIEW THE DOCUMENTIntroduction
VIEW THE DOCUMENTSteps to follow - Hatua za kutengeneza
VIEW THE DOCUMENTSteps to take - Hatua utakazochukua
VIEW THE DOCUMENTKitchen Management - Usimamizi Bora wa Jikoni
VIEW THE DOCUMENTEnergy Saving Tips - Mawaidha ya Kuokoa Kuni
VIEW THE DOCUMENTStove Maintenance - Masimamizi Ya Jiko
VIEW THE DOCUMENTBack Cover - Kinyume

Steps to take - Hatua utakazochukua

Put everything near the site of your new Maendeleo Jiko, the best place is where you cook with the three stones

Weka kila chombo karibu na pahali utakapojengea jiko lako. Pahali bora zaidi kwa shughuli hii ni pale kuna liie jiko la mawe matatu

Level the floor where you are going to put your jiko, and sprinkle it with water to make it damp but not muddy.

Sakafu ya pahali utakapojengea jiko lako ni lazima iwe tambarare, halafu upanyunyizie maji bila kupafanya kuwa na matope

Put the jiko liner in a sufuria of water to get it wet all over.

Hatua ya pili ni kuuweka mjengo wa Jiko la Maendeleo ndani ya sufuria ya maji mpaka liloweke kabisa

Mix the soil and ash properly with a shovel, and then sprinkle it with handfuls of water, mixing all the time, just like making cement. The best way to do this is to have one person turning the soil, and the other throwing on the water.

Halafu changanya udongo na majivu sawasawa ukitumia mwiko wa kujengea. Teka maji kwa mkono ili unyunyize katika mchanganyiko wa udongo na majivu na uendelee kukoroga kama vile ukorogavyo sementi. Njia bora kufanya hivyo ni kuwa na mtu mmoja akoroge udongo na mwengine anyunyize maji.

Now you must find our if you’ve prepared the soil properly.

Test it by squeezing a handful of wet soil into a bail, and dropping it onto the ground from your hip.

If the ball falls and breaks, it is too dry. so you will have to add more water.

If it collapses into mud it is too wet, so more soil will be needed. The ball must hold firm.

Hakikisha umetayarisha udongo sawasawa.

Ujaribu kwa kufinya kibonge cha udongo uwe mviringo au mpira, kisha uangushe kibonge hicho kutoka umbali wa kufikia kiuno chako.

Ikiwa mpira utapasuka, basi udongo ni ukavu zaidi, na kwa hivyo lazima uongeze maji.

Na ikiwa kibonge cha udongo kitajikunja kama matope, basi uko mororo zaidi, na kwa hivyo itakubidi uongeze udongo na mchanga.

Kibonge cha udongo lazima kiwe imara.

Measure a space of at least two flat hands away from the wall, check that the liner is still wet, and place it wide side down on the floor outside that space.

Draw a circle around the liner with a stick, or with your finger. Then place your hands flat on the floor again, against that line, and mark it. Remove the liner.

Pima nafasi ya viganja vya mkono viwili kutoka ukutani, na hakikisha mjengo wa jiko la mabati bado unazizima, halafu uulaze kwa upande wake wa mbavuni katika sakafu mbali na nafasi ulioitenga.

Baadaye chora mviringo kuzunguka ule mjengo ukitumia kijiti au kidole. Halafu weka viganja vya mkono sakafunitena, karibu sana na msitari uliochora, ili uweke alama nyengine. Halafu ondoa mjengo wa jiko la mabati.

Wet some flat stones in a sufuria and, starting from the outside.

Nyunyizia mawe yaliyo sambamba ndani ya sufuria, na kwa kuanza kwa upande wa nje

put them in the inside circle, making sure that no stone is on top of another one.

Weka mawe hayo ndani ya ule mviringo uliochora. Hakikisha hakuna jiwe litakalo lala juu ya lengine

Slap wet soil into the gaps and push everything down hard.

Pachika udongo ulio maji katika mapengo na kisha ufinye kila sehemu chini kwa nguvu.

Then cover the stones thickly with soil, and beat firmly with a panga.

Halafu funika mawe kwa udongo mwingi na upigepige kwa panga ill ushikamane

Sokota vibonge vya udongo katika mkono wako, halafu uvisukume imara kuzunguka sehemu ya nje. Tayari utakuwa umejenga msingi wa Jiko lako la Maendeleo.

Roll soil balls in your hands, and push them in hard around the outside. This is the foundation of your Maendeleo Jiko.

To make sure your cooking sufurias will stand straight on the jiko, put a sufuria on the liner just as if you were going to cook with it, and pour in some clean water. Push the liner into the foundation until the water in the sufuria is level.

Kwa kuhakikisha sufuria yako ya kupikia itakaa vyema juu ya jiko, basi weka sufuria juu ya mjengo wa jiko la mabati kama vile ukitaka kupika nalo, kisha uweke maji safi. Gandamiza mjengo huo katika ule msingi wa jiko uliojenga mpaka maji yawe tambarare

Get some more flat wet stones, and fill the outside circle just like you did the inner one. Leave the door way open wide.

Chukua mawe sambamba mengine halafu ujaze mviringo wa nje kama vile ulivyojaza mviringo wa ndani. Wacha mlango wazi kabisa.

Your jiko liner is in place now, so don’t lean on it. Add the rounded stones. Its very simple. First add the stones, then fill the gaps with the prepared soil mix and put on a thick layer of prepared soil.

Mjengo wa jiko lako uko tayari sasa na kwa hivyo usiutegemee. Ongeza yale mawe ya mviringo. Kwanza ongeza mawe, halafu ziba mapengo na mchanganyiko wa udongo uliotayarishwa maalum kisha unene kwa utaratibu.

Three layers of stone and soil should be enough to bring the outside wall level with the top of your jiko liner, but the wall height depends on what you are going to cook on your jiko. Women who cook ugali every day prefer a low wall, those cooking githeri like it higher.

Miraba mitatu ya udongo na mawe yanatosha kufanya ukuta wa nje ya juu ya mjengo wa jiko lako. Lakini urefu wa ukuta utategemea na kile utakuwa ukipika juu ya jiko lako. Wanawake wapikao ugali kila siku hupendelea ukuta ulio chini kiasi, hali wale wapikao githeri hupendelea ukuta ulio juu kidogo.

Don’t forget to finish the outside with mud balls at each level. Then level the jiko top and sides firmly with a panga.

Usisahau kumaliza kujenga nje ya jiko lako kwa vibonge vya udongo kila hatua. Baadaye fanya upande wa juu wa jiko na mbavuni laini ukitukia panga.

There’s just one more thing to do before you leave your jiko to dry for three days. Air must be able to flow freely so that your Maendeleo Jiko does its work properly and saves kuni. A tongue to support the firewood will give you this free air flow.

Utatakikana kufanya jambo la mwisho kabla kuacha jiko lako likauke kwa siku tatu. Hewa inapaswa kuingia kwa urahisi ili Jiko la Maendeleo liweze kufanya kazi nzuri ya kutumia kuni kidogo. Jukwaa la kushikilia kuni litawezesha hewa kuingia na kutoka kwa urahisi.

Flatten the grate both inside and outside. And put down more wet flat stones a hand’s length away from the fire opening and a thumb’s distance away from the stove sides.

Lainisha kitu cha kushikilia kuni kwa upande wa nje na ndani, na uweke mawe ya sambamba zaidi yenye kuzizima kiganja cha mkono kimoja kutoka palipo mlango wa kuwashia moto, na umbali usiozidi kidole gumba kutoka mbavu za jiko.

Build the stones up on the outside so that they will hold your firewood up at an angle. The stones must be at least three fingers high. Cover the stones with soil, and beat with a panga.

Jenga mawe hayo nje ya mjengo ili yaweze kushikilia kuni zako kwa pembeni. Hakikisha mawe hayo yana urefu wa vidole vitatu. Funika mawe kwa udongo halafu usambaze kwa panga.

When your stove is completely dry, you might like to smear it with a mixture of ash and cowdung, or ash and cement. If you do, it will need another three days, a week altogether, to dry before you light your cooking fire.

Wakati jiko lako limekauka kabisa, unaweza kulipaka na mchanganyiko wa majivu na kinyeshi au mavi ya ng’ombe, au majivu na sementi. Ikiwa utafanya hivyo, litahitaji siku tatu zaidi au juma moja kukauka, kabla kuwasha moto wako wa kupikia.

TO PREVIOUS SECTION OF BOOK TO NEXT SECTION OF BOOK